Yeremia 48:19-27 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Enyi wakazi wa Aroeri,simameni kando ya njia mtazame!Mwulizeni anayekimbia na anayetoroka:‘Kumetokea nini?’

20. Moabu imeaibishwa maana imevunjwa;ombolezeni na kulia.Tangazeni kando ya mto Arnoni,kwamba Moabu imeharibiwa kabisa.

21. “Hukumu imeifikia miji iliyo nyanda za juu: Holoni, Yasa, Mefaathi,

22. Diboni, Nebo, Beth-diblathaimu,

23. Kiriathaimu, Beth-gamuli, Beth-meoni,

24. Keriothi na Bosra. Naam, hukumu imeifikia miji yote ya Moabu mbali na karibu.

25. Nguvu za Moabu zimevunjiliwa mbali na uwezo wake umevunjwa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

26. “Mlewesheni Moabu kwa sababu alijikuza dhidi yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Moabu atagaagaa katika matapishi yake na watu watamcheka.

27. Kumbuka Moabu ulivyomcheka Israeli. Je, alikamatwa pamoja na wezi, hata ukawa unatikisa kichwa chako kila ulipoongea juu yake?

Yeremia 48