Yeremia 48:14-25 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Mwawezaje kusema: ‘Sisi ni mashujaa,na watu wenye nguvu nyingi za vita?’

15. Mwangamizi wa Moabu na miji yake amewasilivijana wake wazuri wamechinjwa.Nimesema mimi mfalmeniitwaye Mwenyezi-Mungu wa Majeshi.

16. Janga la Moabu limekaribia,maangamizi yake yanawasili haraka.

17. Mwomboleezeni Moabu, enyi jirani zake wote,na nyote mnaomjua vizurisemeni: ‘Jinsi gani fimbo ya nguvu ilivyovunjwa,naam fimbo ile ya fahari!’

18. Enyi wenyeji wa Diboni:Shukeni kutoka mahali penu pa fahari,mkaketi katika ardhi isiyo na maji.Maana mwangamizi wa Moabu,amefika kuwashambulia;amekwisha haribu ngome zenu.

19. Enyi wakazi wa Aroeri,simameni kando ya njia mtazame!Mwulizeni anayekimbia na anayetoroka:‘Kumetokea nini?’

20. Moabu imeaibishwa maana imevunjwa;ombolezeni na kulia.Tangazeni kando ya mto Arnoni,kwamba Moabu imeharibiwa kabisa.

21. “Hukumu imeifikia miji iliyo nyanda za juu: Holoni, Yasa, Mefaathi,

22. Diboni, Nebo, Beth-diblathaimu,

23. Kiriathaimu, Beth-gamuli, Beth-meoni,

24. Keriothi na Bosra. Naam, hukumu imeifikia miji yote ya Moabu mbali na karibu.

25. Nguvu za Moabu zimevunjiliwa mbali na uwezo wake umevunjwa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Yeremia 48