4. Hiyo ni siku ya kuwaangamiza Wafilisti wote,kukomesha msaada uliobakia kutoka Tiro na Sidoni.Maana Mwenyezi-Mungu anawaangamiza Wafilisti,watu waliosalia wa kisiwa cha Kaftori.
5. Watu wa Gaza wamenyoa upara kuomboleza;mji wa Ashkeloni umeangamia.Enyi watu wa Anakimu mliobakimpaka lini mtajikatakata kwa huzuni?
6. Ee upanga wa Mwenyezi-Mungu!Utachukua muda gani ndipo utulie?Ingia katika ala yako,ukatulie na kunyamaa!
7. Lakini utawezaje kutulia,hali Mwenyezi-Mungu ameupa kazi?Ameuamuru ushambulie mji wa Ashkelonina watu wanaoishi pwani.”