Yeremia 46:12-16 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Mataifa yamesikia aibu yenu,kilio chenu kimeenea duniani kote;mashujaa wamegongana wenyewe kwa wenyewe,wote pamoja wameanguka.

13. Neno ambalo Mwenyezi-Mungu alimwambia Yeremia wakati alipofika Nebukadneza mfalme wa Babuloni kuishambulia nchi ya Misri:

14. “Tangaza nchini Misri,piga mbiu huko Migdoli,tangaza huko Memfisi na Tahpanesi.Waambie: ‘Kaeni tayari kabisamaana upanga utawaangamiza kila mahali.’

15. Kwa nini shujaa wako amekimbia?Mbona fahali wako hakuweza kustahimili?Kwa sababu mimi Mwenyezi-Mungu nilimwangusha chini!

16. Wengi walijikwaa, wakaanguka,kisha wakaambiana wao kwa wao:‘Simameni, tuwaendee watu wetu,turudi katika nchi yetu,tuukimbie upanga wa adui.’

Yeremia 46