9. Mtu atakayebaki mjini humu atauawa kwa upanga au kwa njaa au kwa maradhi mabaya. Lakini mtu atakayetoka nje ya mji na kujisalimisha kwa Wakaldayo wanaouzingira mji, ataishi; naam, atayanusurisha maisha yake.
10. Nimeamua kuuletea mji huu maafa na sio mema, nasema mimi Mwenyezi-Mungu. Nitautia mikononi mwa mfalme wa Babuloni, naye atauteketeza kwa moto.
11. “Utaiambia jamaa ya mfalme wa Yuda: Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu,