5. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Alaaniwe mtu anayemtegemea binadamu,mtu ambaye anategemea nguvu za binadamu,mtu ambaye moyo wake umeniacha mimi Mwenyezi-Mungu.
6. Huyo ni kama kichaka jangwani,hataona chochote chema kikimjia.Ataishi mahali pakavu nyikani,katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
7. “Abarikiwe mtu anayemtegemea Mwenyezi-Mungu,mtu ambaye Mwenyezi-Mungu ndiye tegemeo lake.
8. Huyo ni kama mti uliopandwa kando ya maji,upenyezao mizizi yake karibu na chemchemi.Hauogopi wakati wa joto ufikapo,majani yake hubaki mabichi.Hauhangaiki katika mwaka wa ukame,na hautaacha kuzaa matunda.
9. “Moyo wa mtu ni mdanganyifu kuliko vitu vyote;hauwezi kuponywa, hakuna awezaye kuuelewa!