Yeremia 17:15-17 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Tazama watu wanavyoniambia:“Jambo alilotishia Mwenyezi-Mungu liko wapi?Acha basi lije!”

16. Sikuikimbia huduma yako ya kuwa mchungajiwala sikutamani ile siku ya maafa ije.Wewe mwenyewe wajua nilichosema kwa mdomo wangu,nilichotamka wakijua waziwazi.

17. Usiwe tisho kwangu;wewe ndiwe kimbilio langu siku ya maafa.

Yeremia 17