Yeremia 13:25-27 Biblia Habari Njema (BHN)

25. Mwenyezi-Mungu asema:“Hayo ndiyo yatakayokupata,ndivyo nilivyoamua kukutenda mimi Mwenyezi-Mungu,kwa sababu umenisahau mimi,ukaamini miungu ya uongo.

26. Nitalipandisha vazi lako hadi kichwanina aibu yako yote itaonekana wazi.

27. Nimeyaona machukizo yako:Naam, uzinifu wako na uzembe wako,na uasherati wako wa kupindukia,juu ya milima na mashambani.Ole wako ee Yerusalemu!Mpaka lini utakaa bila kutakaswa?”

Yeremia 13