Wimbo Ulio Bora 6:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ewe mwanamke uliye mzuri sana;amekwenda wapi huyo mpenzi wako?Ameelekea wapi mpenzi wakoili tupate kushirikiana nawe katika kumtafuta?

2. Mpenzi wangu amekwenda bustanini mwake,mahali ambapo rihani hustawi.Yeye analisha kondoo wakena kukusanya yungiyungi.

3. Mimi ni wake mpenzi wangu, naye ni wangu;yeye huwalisha kondoo wake penye yungiyungi.

Wimbo Ulio Bora 6