8. Nawasihini, enyi wanawake wa Yerusalemu,mkimwona mpenzi wangu,mwelezeni kwamba naugua kwa mapenzi!
9. Ewe upendezaye kuliko wanawake wote!Kwani huyo mpenzi wako ana nini cha zaidi ya mpenzi mwingine,hata utusihi kwa moyo kiasi hicho?
10. Mpenzi wangu ni mzuri na mwenye nguvu,mashuhuri miongoni mwa wanaume elfu kumi.
11. Kichwa chake kizuri kama dhahabu safi,nywele zake ni za ukoka,nyeusi ti kama kunguru.
12. Macho yake ni kama ya hua kandokando ya kijito,ni kama njiwa waliooga maziwa kando ya kijito.
13. Mashavu yake ni kama matuta ya rihanikama bustani iliyojaa manukato na manemane.Midomo yake ni kama yungiyungi,imelowa manemane kwa wingi.