13. Machipukizi yako ni bustani ya mikomamangapamoja na matunda bora kuliko yote,hina na nardo.
14. Nardo na zafarani, mchai na mdalasinimanemane na udi,na mimea mingineyo yenye harufu nzuri.
15. U chemchemi ya bustani,kisima cha maji yaliyo hai,vijito vitiririkavyo kutoka Lebanoni.
16. Vuma, ewe upepo wa kaskazi,njoo, ewe upepo wa kusi;vumeni juu ya bustani yangu,mlijaze anga kwa manukato yake.Mpenzi wangu na aje bustanini mwake,ale matunda yake bora kuliko yote.