Wimbo Ulio Bora 1:12-15 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Mfalme alipokuwa kwenye kochi lake,marashi yangu ya nardo yalisambaa kila mahali.

13. Mpenzi wangu ni kama mfuko wa manemane kwangu,kati ya matiti yangu.

14. Mpenzi wangu ni kama maua ya hina yachanuayo,kwenye mashamba ya mizabibu huko Engedi.

15. Hakika u mzuri, ee mpenzi wangu,hakika u mzuri!Macho yako ni kama ya hua!

Wimbo Ulio Bora 1