16. Lakini wote hawakuipokea hiyo habari njema. Maana Isaya alisema: “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?”
17. Hivyo basi, imani inatokana na kuusikia ujumbe, na huo ujumbe unatokana na neno la Kristo.
18. Lakini nauliza: Je, hawakuusikia huo ujumbe? Naam, waliusikia; kama Maandiko Matakatifu yasemavyo:“Sauti yao imeenea duniani kote;maneno yao yamefika mpaka kingo za ulimwengu.”
19. Tena nauliza: Je, yawezekana kwamba watu wa Israeli hawakufahamu? Mose mwenyewe ni wa kwanza kujibu:“Nitawafanyeni muwaonee wivuwatu ambao si taifa;nitawafanyeni muwe na hasirajuu ya taifa la watu wapumbavu.”
20. Tena Isaya anathubutu hata kusema:“Wale ambao hawakunitafuta wamenipata;nimejionesha kwao wasiouliza habari zangu.”
21. Lakini kuhusu Israeli anasema:“Mchana kutwa niliwanyoshea mikono yangu watu waasi na wasiotii.”