1. “Kama mtu yeyote akitakiwa kutoa ushahidi kwenye baraza juu ya jambo aliloona au kulisikia naye akakataa kusema kitu, basi, huo ni uovu na atauwajibikia.
2. Au kama mtu yeyote miongoni mwenu amekuwa najisi bila kukusudia kwa kugusa kitu chochote najisi, iwe ni mzoga wa mnyama wa porini au wa kufugwa au wadudu, atakuwa na hatia.
3. Au mtu akigusa chochote kilicho najisi cha binadamu, kiwe kiwacho, ambacho humfanya mtu kuwa najisi, naye hana habari, basi, atakapojua atakuwa na hatia.
4. Au, kama mtu akiapa kufanya chochote kile, chema au kibaya, kama wafanyavyo watu bila kufikiri, atakapojua atakuwa na hatia.
5. Basi, mtu akiwa na hatia kuhusu mambo hayo lazima akiri dhambi yake aliyotenda
6. na kumletea Mwenyezi-Mungu sadaka yake ya kuondoa hatia. Kwa ajili ya dhambi aliyotenda ataleta kondoo jike au mbuzi jike kutoka kundi lake amtoe sadaka kwa ajili ya kuondoa dhambi. Naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake.
7. “Lakini kama hawezi kutoa mwanakondoo wa sadaka ya kuondoa hatia kwa ajili ya dhambi aliyotenda, basi atamletea Mwenyezi-Mungu hua wawili au makinda mawili ya njiwa: Mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi, na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.
8. Atawaleta kwa kuhani, naye kuhani atamtoa mmoja awe sadaka ya kuondoa dhambi kwa kumkongonyoa shingo yake bila kukichopoa kichwa chake.