Walawi 18:7-16 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Kamwe usimvunjie heshima baba yako kwa kulala na mama yako aliyekuzaa. Usimwaibishe; yeye ni mama yako.

8. Kamwe usimvunjie heshima baba yako kwa kulala na mmoja wa wake zake. Hao ni mama zako.

9. Kamwe usilale na dada yako, awe ni dada yako halisi au dada yako wa kambo.

10. Kamwe usilale na mjukuu wako, mtoto wa mwanao au binti yako; maana sehemu zao za siri ni kama zako mwenyewe.

11. Kamwe usilale na msichana aliyezaliwa na mama yako wa kambo aliyeolewa na baba yako; msichana huyo ni dada yako.

12. Kamwe usilale na shangazi yako; kwani huyo ni dada wa baba yako.

13. Kamwe usilale na dada wa mama yako; kwani huyo ni mama yako mkubwa au mdogo.

14. Kamwe usilale na mke wa baba yako mkubwa au mdogo; huyo ni mama yako.

15. Kamwe usilale na mke wa mwanao; huyo ni mkewe mwanao. Kamwe usilale naye.

16. Kamwe usilale na mke wa ndugu yako; huyo ni shemeji yako.

Walawi 18