Walawi 18:28-30 Biblia Habari Njema (BHN)

28. Basi, nyinyi msifanye mambo hayo, la sivyo nchi hiyo itawatapika kama ilivyolitapika taifa lililokuwa kabla yenu.

29. Watu wote watakaofanya mambo hayo ya kuchukiza ni lazima watengwe mbali na watu wao.

30. Kwa hiyo shikeni kikamilifu yote ninayowaagiza; msifuate mazoea yoyote ya kuchukiza yaliyofanywa na wale walioishi nchini kabla yenu, msije mkajitia unajisi kwayo. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.”

Walawi 18