Walawi 18:21-23 Biblia Habari Njema (BHN)

21. “Kamwe usimtoe mtoto wako yeyote kuwa sadaka kwa mungu Moleki maana kufanya hivyo utalikufuru jina langu mimi Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.

22. “Kamwe usilale na mwanamume mwenzio kana kwamba ni mwanamke. Hilo ni chukizo.

23. Kamwe usilale na mnyama ili usijitie najisi; mwanamume au mwanamke yeyote kamwe asifanye hivyo; kufanya hivyo ni upotovu.

Walawi 18