Waebrania 8:8-13 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Lakini Mungu aliwalaumu watu wake aliposema:“Siku zinakuja, asema Bwana,ambapo nitafanya agano jipyana watu wa Israeli na wa Yuda.

9. Agano hili halitakuwa kama lile nililofanya na babu zaosiku nilipowaongoza kwa mkono kutoka Misri.Hawakuwa waaminifu kwa agano langu;na hivyo mimi sikuwajali, asema Bwana.

10. Hili ndilo agano nitakalofanya na watu wa Israeli siku zijazo, asema Bwana:Nitaweka sheria zangu akilini mwao,na kuziandika mioyoni mwao.Mimi nitakuwa Mungu wao,nao watakuwa watu wangu.

11. Hakuna atakayemfundisha mwananchi mwenzake,wala atakayemwambia ndugu yake:‘Mjue Bwana’.Maana wote, wadogo na wakubwa, watanijua mimi.

12. Nitawasamehe makosa yao,wala sitakumbuka tena dhambi zao.”

13. Kwa kusema juu ya agano jipya, Mungu alilichakaza lile la kwanza; na chochote kinachochakaa na kuwa kikuukuu kitatoweka karibuni.

Waebrania 8