Ufunuo 21:25-27 Biblia Habari Njema (BHN)

25. Milango ya mji huo itakuwa wazi mchana wote; maana hakutakuwa na usiku humo.

26. Fahari na utajiri wa watu wa mataifa utaletwa humo ndani.

27. Lakini hakuna chochote kilicho najisi kitakachoingia humo; wala mtu yeyote atendaye mambo ya kuchukiza au ya uongo hataingia humo. Ni wale tu walioandikwa katika kitabu cha uhai cha Mwanakondoo ndio watakaoingia ndani.

Ufunuo 21