Tito 2:4-9 Biblia Habari Njema (BHN)

4. ili wawazoezeshe kina mama vijana kuwapenda waume zao na watoto,

5. wawe na kiasi na safi, waangalie vizuri mambo ya nyumbani, na wawatii waume zao, ili ujumbe wa Mungu usije ukadharauliwa.

6. Kadhalika, wahimize vijana wawe na kiasi.

7. Katika mambo yote wewe mwenyewe unapaswa kuwa mfano wa matendo mema. Uwe mnyofu na uwe na uzito katika mafundisho yako.

8. Maneno yako yasiwe na hitilafu yoyote ili maadui zako waaibike wasipopata chochote kibaya cha kusema juu yetu.

9. Watumwa wanapaswa kuwatii wakuu wao na kuwapendeza katika mambo yote. Wasibishane nao,

Tito 2