Ruthu 1:11-16 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Naye Naomi akawasihi, “Rudini, binti zangu. Kwa nini kunifuata? Je, mnafikiri naweza kupata tena watoto watakaokuwa waume zenu?

12. Rudini nyumbani kwenu binti zangu, kwa maana mimi ni mzee mno, siwezi kuolewa tena. Hata kama ningesema ninalo tumaini, na hata kama ningepata mume usiku huu na kupata watoto,

13. je, mngeweza kungoja mpaka wakue? Je, mngeweza kujizuia msiolewe na waume wengine? Sivyo, binti zangu! Mambo yangu ni magumu mno kwa ajili yenu, maana Mwenyezi-Mungu amenipiga kipigo.”

14. Hapo walipaza sauti wakaanza kulia tena. Ndipo Orpa akamkumbatia mkwewe, akamuaga na kurudi nyumbani; lakini Ruthu, akaandamana naye.

15. Basi Naomi akamwambia, “Ruthu, tazama dada yako amerudi nyumbani kwake na kwa mungu wake; basi, nawe pia urudi, umfuate dada yako.”

16. Lakini Ruthu akamjibu,“Usinisihi nikuache wewe,wala usinizuie kufuatana nawe.Kokote utakakokwenda ndiko nami nitakakokwenda,na ukaapo nitakaa,watu wako watakuwa watu wangu,na Mungu wako atakuwa Mungu wangu.

Ruthu 1