Nehemia 12:8-23 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Walawi: Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda na Matania, ambaye alihusika na usimamizi wa nyimbo za shukrani akishirikiana na ndugu zake.

9. Nao Bakbukia na Uno rafiki zao, walisimama ibadani mkabala nao.

10. Yeshua alimzaa Yoyakimu, Yoyakimu alimzaa Eliashibu, Eliashibu alimzaa Yoyada,

11. Yoyada alimzaa Yonathani na Yonathani akamzaa Yadua.

12. Yoyakimu alipokuwa kuhani mkuu, makuhani wafuatao walikuwa wakuu wa koo zao: Wa Seraya, Meraya; wa Yeremia, Hanania;

13. wa Ezra, Mehulamu; wa Amaria, Yehohanani;

14. wa Maluki, Yonathani; wa Shebania, Yosefu;

15. wa Harimu, Adna; wa Merayothi, Helkai;

16. wa Ido, Zekaria; wa Ginethoni, Meshulamu;

17. wa Abiya, Zikri; ukoo wa Miniamini; wa Moadia, Piltai;

18. wa Bilga, Shamua; wa Shemaya, Yehonathani;

19. wa Yoaribu, Matenai; wa Yedaya, Uzi;

20. wa Salai, Kalai; wa Amoki, Eberi;

21. wa Hilkia, Heshabia; na wa ukoo wa Yedaya, Nethaneli.

22. Wakati wa Eliashibu, Yoyada, Yohanani na Yadua wakuu wa jamaa za Walawi, waliorodheshwa; vilevile wakati wa utawala wa mfalme Dario wakuu wa jamaa za makuhani waliorodheshwa.

23. Wakuu wa jamaa za ukoo wa Lawi waliorodheshwa katika kitabu cha Kumbukumbu mpaka wakati wa Yohanani mjukuu wa Eliashibu.

Nehemia 12