12. Simba dume amewararulia watoto wake nyama ya kutosha,akawakamatia simba majike mawindo yao;ameyajaza mapango yake mawindo,na makao yake mapande ya nyama.
13. Tazama, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nitapambana nawe: Nitayateketeza kwa moto magari yako ya farasi, nitawamaliza kwa upanga hao simba wako vijana, nyara ulizoteka nitazitokomeza kutoka nchini, na sauti ya wajumbe wako haitasikika tena.