Mwanzo 49:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Yakobo akawaita wanawe, akasema, “Kusanyikeni pamoja niwaambieni mambo yatakayowapata siku zijazo.

2. “Kusanyikeni msikie, enyi wana wa Yakobo,nisikilizeni mimi Israeli, baba yenu.

3. “Wewe Reubeni ni mzaliwa wangu wa kwanza,nguvu yangu na tunda la ujana wangu.Wewe wawapita ndugu zako kwa ukuu na nguvu.

Mwanzo 49