16. Gadi na wanawe: Sifioni, Hagi, Shuni, Esboni, Eri, Arodi na Areli.
17. Asheri na wanawe: Imna, Ishva, Ishvi, Beria na Sera, dada yao. Beria na wanawe: Heberi na Malkieli.
18. Hawa kumi na sita ni watoto na wajukuu wa Yakobo na Zilpa, mjakazi ambaye Labani alimpa Lea, binti yake.
19. Raheli alimzalia Yakobo wana wawili: Yosefu na Benyamini.
20. Huko Misri, Asenathi, binti Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni, alimzalia Yosefu wana wawili: Manase na Efraimu.
21. Wana wa Benyamini walikuwa Bela, Bekeri, Ashbeli, Gera, Naamani, Ehi, Roshi, Mupimu, Hupimu na Ardi.
22. Watu hao kumi na wanne ni watoto na wajukuu wa Yakobo na Raheli, mkewe.
23. Dani na Hushimu, mwanawe.
24. Naftali na wanawe: Yaseeli, Guni, Yeseri na Shilemu.
25. Hao saba ni watoto na wajukuu wa Yakobo na Bilha, mjakazi ambaye Labani alimpa binti yake Raheli.
26. Jumla ya wazawa wa Yakobo aliokwenda nao Misri, bila kuwahesabu wake za wanawe, ilikuwa watu sitini na sita.