14. Zebuluni na wanawe: Seredi, Eloni na Yaleeli.
15. Hao ndio wana ambao Lea alimzalia Yakobo kule Padan-aramu, pamoja na Dina binti yake. Jumla ya wanawe, binti zake na wajukuu wake walikuwa watu thelathini na watatu.
16. Gadi na wanawe: Sifioni, Hagi, Shuni, Esboni, Eri, Arodi na Areli.
17. Asheri na wanawe: Imna, Ishva, Ishvi, Beria na Sera, dada yao. Beria na wanawe: Heberi na Malkieli.