Mwanzo 37:21-26 Biblia Habari Njema (BHN)

21. Lakini Reubeni aliposikia maneno hayo, akataka kumwokoa mikononi mwao; basi akawaambia ndugu zake, “Tafadhali, tusimuue.

22. Msimwage damu. Ila mtumbukizeni katika shimo hili hapa mbugani, lakini msimdhuru.” Alisema hivyo kusudi aweze kumwokoa Yosefu mikononi mwao, na baadaye amrudishe kwa baba yake.

23. Yosefu alipowafikia ndugu zake, wao wakamvua kanzu yake.

24. Kisha wakamshika na kumtupa shimoni. Lakini shimo hilo halikuwa na maji.

25. Walipoketi kula, wakaona msafara wa Waishmaeli wakisafiri kutoka Gileadi kwenda Misri. Ngamia wao walikuwa wamebeba ubani, zeri na manemane.

26. Hapo Yuda akawaambia ndugu zake, “Tutapata faida gani tukimuua ndugu yetu na kuficha mauaji yake?

Mwanzo 37