Mwanzo 23:12-18 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Abrahamu akainama tena kwa heshima mbele ya wananchi,

13. akamwambia Efroni, wananchi wote wakisikia, “Nakuomba, tafadhali unisikilize. Nitakulipa bei kamili ya shamba lako, na ninakuomba upokee malipo haya, ili nipate kumzika humo marehemu mke wangu.”

14. Efroni akamjibu Abrahamu, “Bwana, nisikilize;

15. shamba lenye thamani ya shekeli 400 tu za fedha ni nini kati yako na mimi? Mzike marehemu mke wako.”

16. Abrahamu akakubaliana na Efroni, akampimia kiasi cha fedha alichotaja mbele ya Wahiti wote, fedha shekeli 400, kadiri ya vipimo vya wafanyabiashara wa wakati huo.

17. Basi, shamba la Efroni lililoko huko Makpela, mashariki ya Mamre, pango na miti yote iliyokuwamo pamoja na eneo zima, likawa lake

18. Abrahamu mbele ya Wahiti wote waliokutanika penye lango la mji.

Mwanzo 23