Mwanzo 19:35-37 Biblia Habari Njema (BHN)

35. Basi, usiku huo pia wakamlevya baba yao kwa divai, kisha yule binti mdogo akaenda akalala naye. Lakini baba yake hakujua wakati bintiye alipolala naye, wala alipoondoka.

36. Hivyo, binti wote wawili wa Loti wakapata mimba kutokana na baba yao.

37. Yule binti wa kwanza akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Moabu. Huyo ndiye baba wa Wamoabu hadi leo.

Mwanzo 19