Mwanzo 13:16-18 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Wazawa wako nitawafanya wawe wengi wasiohesabika, kama vile mavumbi ya nchi yasivyoweza kuhesabika!

17. Basi, inuka uitembelee nchi hii katika mapana na marefu, kwani nitakupa wewe.”

18. Kwa hiyo, Abramu akangoa hema, akaenda kukaa karibu na mialoni ya Mamre kule Hebroni; huko akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu.

Mwanzo 13