5. Usimwamini mwenzako,wala usimtumainie rafiki yako.Chunga unachosema kwa mdomo wako,hata na mke wako wewe mwenyewe.
6. Maana, mtoto wa kiume anamdharau baba yake;mtoto wa kike anashindana na mama yake,mke wa mwana anapingana na mama mkwe wake.Maadui wa mtu ni watu wa nyumbani mwake.
7. Lakini mimi namtumainia Mwenyezi-Mungu,namtazamia Mungu mwenye kuniokoa;Mungu wangu atanisikiliza.
8. Usifurahie maafa yangu ewe adui yangu!Nikianguka, nitainuka tena;Nikiwa gizani, Mwenyezi-Mungu ni mwanga wangu.
9. Kwa vile nimemkosea Mwenyezi-Mungu,sina budi kuvumilia ghadhabu yake,mpaka atakapotetea kisa changuna kunijalia haki yangu.Atanileta nje kwenye mwanga,nami nitaona akithibitisha haki.
10. Hapo adui yangu ataona hayonaye atajaa aibu;maana aliniambia: “Wapi basi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako?”Mimi mwenyewe nitamwona adui akianguka;atakanyagwakanyagwa chini kama tope la njiani.
11. Siku yaja ambapo kuta za mji wenu zitajengwa upya.Siku hiyo mipaka ya nchi yenu itapanuliwa.