3. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Enyi watu wangu, nimewatendea nini?Nimewachosha kwa kitu gani?Nijibuni!
4. Mimi niliwatoa nchini Misri;niliwakomboa kutoka utumwani;niliwapeni Mose, Aroni na Miriamu kuwaongoza.
5. Enyi watu wangu,kumbukeni njama za Balaki mfalme wa Moabu,na jinsi Balaamu mwana wa Beori alivyomjibu.Kumbukeni yaliyotukia njiani kati ya Shitimu na Gilgali.Kumbukeni mtambue matendo yangu ya kuwaokoa!”
6. Nimwendee Mwenyezi-Mungu na kitu gani,nipate kumwabudu Mungu aliye juu?Je, nimwendee na sadaka za kuteketezwa,nimtolee ndama wa mwaka mmoja?
7. Je, Mwenyezi-Mungu atapendezwanikimtolea maelfu ya kondoo madume,au mito elfu na elfu ya mafuta?Je, nimtolee mzaliwa wangu wa kwanzakwa ajili ya kosa langu,naam, mtoto wangukwa ajili ya dhambi yangu?