14. Hivyo, mnapaswa kuagana na kuwaacha wakazi wa Morasheth-gathi.Nao mji wa Akzibu hautawasaidia wafalme wa Israeli,
15. Enyi wakazi wa Maresha,Mungu atawaleteeni tena adui atakayewateka.Viongozi waheshimiwa wa Israeliwatakimbilia pangoni huko Adulamu.
16. Enyi watu wa Yuda, nyoeni uparakuwaombolezea watoto wenu wapenzi;panueni upara wenu uwe mpana kama wa tai,maana watoto wenu watawaacha kwenda uhamishoni.