Mhubiri 10:5-10 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Kuna uovu niliogundua hapa duniani, uovu unaosababishwa na watawala:

6. Kwamba wapumbavu wanapewa kazi za madaraka ya juu, na matajiri wanachukua nafasi za mwisho.

7. Nimeona watumwa wanapanda farasi, na wakuu wanatembea kwa miguu kama watumwa.

8. Mchimba shimo hutumbukia mwenyewe,abomoaye ukuta huumwa na nyoka.

9. Mchonga mawe huumizwa nayo,mkata kuni hukabiliwa na hatari.

10. Nguvu nyingi zaidi zahitajikakwa mtumiaji shoka butu lisilonolewa,lakini kutumia hekima humfanya mtu afanikiwe.

Mhubiri 10