18. Kutokana na uvivu wa mtu, paa hubonyea;kwa sababu ya uzembe, nyumba huvuja.
19. Chakula ni kwa ajili ya kujifurahisha,divai huchangamsha maisha;na fedha husababisha hayo yote.
20. Usimwapize mtawala hata moyoni mwako,wala usimwapize tajiri hata chumbani mwako unakolala,kwa kuwa ndege ataisikia sauti yako,au kiumbe arukaye atatangaza maneno yako.