21. Kumbuka njia za mtu zi wazi mbele ya Mwenyezi-Mungu;yeye anaona kila hatua anayochukua binadamu.
22. Mtu mwovu hunaswa kwa uovu wake mwenyewe;hukamatwa katika tanzi za dhambi yake mwenyewe.
23. Yeye hufa kwa utovu wa nidhamu,huangamia kwa sababu ya upuuzi wake mkuu.