15. Mkeo ni kama kisima cha maji safi:Kunywa maji ya kisima chako mwenyewe.
16. Ya nini chemchemi zako zitawanywe mbali,na vijito vya maji barabarani?
17. Hiyo ni yako wewe mwenyewe,wala usiwashirikishe watu wengine.
18. Chemchemi yako na ibarikiwe,umfurahie mke uliyemwoa ukiwa kijana.
19. Ni mzuri kama ayala, apendeza kama paa.Mahaba yake yakufurahishe kila wakati,umezwe daima na pendo lake.