Methali 30:3-8 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Sijajifunza hekima,wala sijui kitu juu ya Mungu Mtakatifu.

4. Ni nani aliyepanda juu mbinguni akashuka chini?Ni nani aliyekamata upepo mkononi?Ni nani aliyefunga maji katika kitambaa?Ni nani aliyeiweka mipaka yote ya dunia?Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe?Niambie kama wajua!

5. Maneno yote ya Mungu ni ya kuaminika;yeye ni ngao yao wote wanaomkimbilia.

6. Usiongeze neno katika maneno yake,asije akakukemea, nawe ukaonekana mwongo.

7. Mambo haya mawili nakuomba ee Mungu,wala usinikatalie kabla sijafa:

8. Uniondolee uongo na udanganyifu;usinipe umaskini wala utajiri;unipatie chakula ninachohitaji,

Methali 30