12. Kuna watu ambao hujiona kuwa wema,kumbe bado hawajatakaswa uchafu wao.
13. Kuna na wengine – kiburi ajabu!Hudharau kila kitu wanachokiona.
14. Kuna watu ambao meno yao ni kama upanga,na magego yao ni kama visu.Wako tayari kuwatafuna maskini wa nchi,na wanyonge walio miongoni mwa watu!
15. Mruba anao binti wawili wasemao, “Nipe, nipe!”Kuna vitu vitatu ambavyo kamwe havishibi,naam, vitu vinne visivyosema, “Imetosha!”
16. Kuzimu,tumbo la mwanamke lisilozaa,ardhi isiyoshiba maji,na moto usiosema, “Imetosha!”
17. Kama mtu akimdhihaki baba yake,na kudharau utii kwa mama yake,kunguru wa bondeni watamdonoa macho,na kuliwa na tai.
18. Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu,naam, mambo manne nisiyoyaelewa:
19. Njia ya tai angani,njia ya nyoka mwambani,njia ya meli baharini,na kinachomvuta mwanamume kwa mwanamke.
20. Mwenendo wa mwanamke mwasherati ni hivi:Yeye hula, akajipangusa mdomo,na kusema, “Sijafanya kosa lolote!”
21. Kuna mambo matatu ambayo huitetemesha dunia,naam, mambo manne ambayo haiwezi kuyastahimili: