Methali 29:15-19 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Adhabu na maonyo huleta hekima,lakini mtoto aliyeachwa afanye apendavyo humwaibisha mama yake.

16. Waovu wakitawala maovu huongezeka,lakini waadilifu watashuhudia kuanguka kwao.

17. Mpe nidhamu mwanao naye hatakupa wasiwasi;yeye ataufurahisha moyo wako.

18. Pasipo maono ya kinabii watu hukosa nidhamu;heri mtu yule anayeshika sheria.

19. Mtumwa haonyeki kwa maneno matupu,maana ingawa anayaelewa yeye hatayatii.

Methali 29