4. Watu wanaovunja sheria huwasifu waovu,lakini wanaoishika sheria hupingana nao.
5. Waovu hawajui maana ya haki,lakini wamchao Mwenyezi-Mungu wanaielewa kabisa.
6. Afadhali maskini aishiye kwa unyofu,kuliko tajiri aishiye kwa upotovu.
7. Mtoto ashikaye sheria ni mwenye hekima,lakini rafiki wa walafi humwaibisha baba yake.
8. Aongezaye mali yake kwa riba na kutoza faidaanamkusanyia mwingine mwenye kuwahurumia maskini.
9. Anayekataa kuisikia sheria,huyo hata sala yake ni chukizo kwa Mungu.
10. Anayemshawishi mtu mwema kutenda mabaya,ataanguka katika shimo lake mwenyewe.Wasio na hatia wamewekewa mema yao.
11. Tajiri hujiona mwenyewe kuwa mwenye hekima,lakini maskini mwenye busara atamfichua.