Methali 28:18-24 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Aishiye kwa unyofu atasalimishwa,lakini mdanganyifu ataanguka kabisa.

19. Anayelima shamba lake atapata chakula kingi,bali anayefuata yasiyofaa atapata umaskini tele.

20. Mtu mwaminifu atapata baraka tele,lakini mwenye pupa ya kuwa tajiri hataepa adhabu.

21. Si vizuri kumbagua mtu;watu hufanya mabaya hata kwa kipande cha mkate.

22. Mtu bahili hukimbilia mali,wala hajui kwamba ufukara utamjia.

23. Amwonyaye mwenzake hatimaye hupata mema zaidi,kuliko yule anayembembeleza kwa maneno matamu.

24. Anayeiba mali ya baba yake au mama yake, akasema si kosa,hana tofauti yoyote na wezi wengine.

Methali 28