20. Kuzimu na Uharibifu kamwe havishibi,kadhalika na macho ya watu hayashibi.
21. Ubora wa fedha au dhahabu hupimwa kwa moto,na mtu hupimwa kutokana na sifa zake.
22. Mtwange mpumbavu katika kinu pamoja na nafaka,lakini hutafaulu kumtenganisha na upumbavu wake.
23. Angalia vizuri hali ya mifugo yako;tunza vizuri wanyama wako.