2. Acha watu wengine wakusifu,kuliko mdomo wako wewe mwenyewe.
3. Jiwe ni zito na mchanga kadhalika,lakini usumbufu wa mpumbavu ni mzito zaidi.
4. Ghadhabu ni katili na hasira huangamiza;lakini ni nani awezaye kuukabili wivu?
5. Afadhali mtu anayekuonya waziwazi,kuliko yule afichaye upendo.