Methali 25:9-16 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Suluhisha ugomvi na mwenzako peke yake,na kila mmoja wenu asitoe siri ya mwenzake;

10. watu wasije wakajua kuna siri,ukajiharibia jina lako daima.

11. Neno lisemwalo wakati unaofaa,ni kama nakshi za dhahabu juu ya madini ya fedha.

12. Onyo la mwenye hekima kwa mtu msikivu,ni bora kuliko pete au vito vya dhahabu safi.

13. Mjumbe mwaminifu humfurahisha yule aliyemtuma,kama maji baridi wakati wa joto la mavuno.

14. Kama vile mawingu na upepo bila mvua,ndivyo alivyo mtu anayejigamba kutoa zawadi asiitoe.

15. Kwa uvumilivu mtawala huweza kushawishika;ulimi laini huvunja mifupa.

16. Upatapo asali kula kiasi cha kukutosha,usije ukaikinai na kuitapika.

Methali 25