Methali 23:20-28 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Usiwe mmoja wa walevi wa divai,wala walafi wenye kupenda nyama,

21. maana walevi na walafi wataishia kuwa maskini,anayetumia siku yake kusinzia atavaa matambara.

22. Msikilize baba yako aliyekuzaa,wala usimdharau mama yako akizeeka.

23. Nunua ukweli, wala usiuuze;nunua hekima, mafunzo na busara.

24. Baba wa mtoto mwadilifu atajaa furaha;anayemzaa mtoto mwenye hekima atamfurahia.

25. Wafurahishe baba na mama yako;mama aliyekuzaa na afurahi.

26. Mwanangu, nisikilize kwa makini,shikilia mwenendo wa maisha yangu.

27. Malaya ni shimo refu la kutega watu;mwanamke mgeni ni kama kisima chembamba.

28. Yeye hunyemelea kama mnyanganyi,husababisha wanaume wengi kukosa uaminifu.

Methali 23