Methali 20:2-7 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Ghadhabu kali ya mfalme ni kama simba angurumaye;anayemkasirisha anayahatarisha maisha yake.

3. Ni jambo la heshima kuepa ugomvi;wapumbavu ndio wanaogombana.

4. Mvivu halimi wakati wa kulima;wakati wa mavuno atatafuta asipate chochote.

5. Fikira za mtu zimefichika kama kilindi cha maji;lakini mtu mwenye busara ajua kuzichota humo.

6. Watu wengi hujivunia kuwa wema,lakini mwaminifu wa kweli apatikana wapi?

7. Mtu mwadilifu akiishi kwa unyofu;watoto wake atakaowaacha watabarikiwa.

Methali 20