Methali 19:6-11 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Watu wengi hujipendekeza kwa wakuu;kila mtu hutaka kuwa rafiki ya mtu mkarimu.

7. Maskini huchukiwa na ndugu zake;marafiki zake ndio zaidi: Humkimbia!Hata awabembeleze namna gani hatawapata.

8. Ajipatiaye hekima anaipenda nafsi yake;anayezingatia busara atastawi.

9. Shahidi mwongo hatakosa kuadhibiwa;asemaye uongo ataangamia.

10. Haifai kwa mpumbavu kuishi kwa anasa,tena ni vibaya zaidi mtumwa kuwatawala wakuu.

11. Mwenye busara hakasiriki upesi;kusamehe makosa ni fahari kwake.

Methali 19