27. Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho,utapotea mara mbali na maneno ya hekima.
28. Shahidi asiyefaa kitu huidhihaki haki;na kinywa cha mwovu hubugia uovu.
29. Adhabu iko tayari kwa wenye mzaha,mijeledi imetayarishwa kuchapa migongo ya wapumbavu.