16. Anayeshika amri anasalimisha maisha yake;anayepuuza agizo atakufa.
17. Anayemsaidia maskini anamkopesha Mwenyezi-Mungu;Mwenyezi-Mungu atamlipa kwa tendo lake jema.
18. Mrudi mwanao kungali bado na tumaini,lakini usimwadhibu kiasi cha kumwangamiza.
19. Mtu wa hasira kali lazima apate adhabu;ukimwachia mara moja itakubidi kumwachia tena.
20. Sikiliza shauri na kupokea mafundisho,upate hekima ya kukufaa siku zijazo.
21. Kichwani mwa mtu mna mipango mingi,lakini anachokusudia Mwenyezi-Mungu ndicho kitakachofanyika.
22. Kinachotakiwa kwa mtu ni uaminifu;afadhali mtu maskini kuliko mtu mwongo.
23. Kumcha Mwenyezi-Mungu kunaleta uhai;amchaye hujaliwa pumziko la kutosheleza,wala hatapatwa na baa lolote.